by Yahaya Jumanne
Crop rotation is an essential technique for soil fertility and pest management in Forest Gardens. To simplify things, we used the rotation from green leafy vegetables to legumes, from legumes to roots, from roots to fruits, and back to green leafy vegetables. This matches somehow with our simplified instruction we also give to farmers of planting three types of vegetables, leaves, roots, and fruits; and as many colours as possible for nutritional benefits.
Below is the lesson plan in Swahili for crop rotation
Mzunguko wa Mazao ya Mbogamboga
- Utangulizi
Kilimo cha mzunguko wa mazao ni aina ya kilimo hai ambacho kinahusisha kulima mazao tofauti tofauti kwa kila msimu wa kilimo kwenye eneo moja. Mfano msimu wa kwanza mkulima akilima Leshuu basi msimu unaofuata itabidi alime zao tofauti na Leshuu inaweza kuwa karoti, bilinganya au bamia
2. Faida za kilimo cha mzunguko wa mazao
- Inaboresha afya ya udongo
- Inapunguza athari na idadi ya visumbufu kama vile magugu, wadudu, virusi na bacteria
- Inaongeza uzalishaji wa zao husika katika msimu unaofuata
- Inaongeza upatikanaji wa mazao zaidi ya moja sokoni
3. Vitu vya kuzingatia unapofanya kilimo cha mzunguko wa mazao
Aina ya zao moja na lingine lazima kuwe na utofauti kati ya zao linalopandwa msimu wa kwanza na wapili. Utofauti huu unaweza kuwa katika:
- Aina ya mizizi: Mazao haya lazima yatofautiane kwenye urefu wa mizizii kama zao moja likiwa na mizizi mirefu basi lingine liwe na mizizi mifupi ili kutofautiana kwenye kuchukua virutubisho kwenye udongo mfano; chainizi na bamia.
- Vinavyo athiri mazao husika. Mazao haya lazima yawe yanatofautiana kwenye aina ya visumbufu vinavyo athiri ili kuvunja mzunguko wa mazaliano na ukuaji wa visumbufu, mfano bamia ina athiriwa na Nzi weusi (Alphids) wakati karoti haiathiriwi na nzi weusi.
- Uhitaji wa maji, lazima kuwe na utofauti wamahitaji ya maji katika mazao yatakayo pandwa kwenye mzunguko. Mfano karoti inahitaji maji mengi kulinganisha na Sukuma wiki hivyo mazao haya yanaweza kupandwa kwenye misimu miwili tofauti ili kuwa na tija kwenye mzunguko.
- Uhitaji wa rotuba tofauti: Mchicha na leshuu huitaji Nitrojeni kwa wingi kwaajili ya ukuaji wa majani, Karoti na kitunguu huitaji potasiamu zaidi kwaajili ya ukuaji wa mizizi.
4. Aina za mzunguko wa mazao
- Majani (yanahitaji kiasi kikubwa cha Nitrojeni): Kabeji, Mchicha, Sukuma, Mnavu, Chainizi
- Matunda (yanahitaji Nitrojeni kidogo, zaidi Fosforasi): Nyaya, Pilipili, Biringanya, bamia, ngongwe
- Mizizi (yanahitaji Nitrojeni kidogo, potasiamu zaidi na Fosforasi kiasi): Karoti, viazi, kitunguu
- Kunde/Maharage (hurejesha Nitrojeni kwenye ardhi): Karanga, soya, mbaazi, kunde

