Encouraging farmers to plant timber, fruit and multipurpose trees in the Forest Garden (plus Lesson plan in Swahili)

by Yahaya Jumanne

Our commitment to increasing biodiversity we have been selecting potential species for various timber trees, fruit trees, and perennial vegetables for some farmers for simple experimenting. Farmers have so far planted Cordia africana, Grevillea robusta, Markhamia lutea, Neem, alongside with fruit trees such as guava, mango, passion, lemon, orange and avocado, Morus alba to diversify their crops. The aim to enrich the agricultural landscape and provide a sustainable source of nutrition and income for the farmers.

Markhamia seedlings
Young cordia tree
Transplanted grevillea seedlings from seedbeds to seedbags
Morus alba start bearing fruits
Cordia seedlings
mango seedlings

Below is a lesson plan in Swahili with the objective of guiding farmers in their efforts to add trees on their farms and getting a proper Forest Garden.

1. Utangulizi

Faida za bustani msitu:

  • kuongeza uzalishaji wa chakula kipindi chote cha mwaka
  • kuboresha lishe
  • kuzalisha malisho kwa wanyama
  • kuzalisha kuni na mbao
  • kupunguza mmomonyoko kwa kufunika udongo
  • kuboresha rutuba ya udongo kwa kufyonza nitrojeni kutoka hewani
  • kuzalisha biomasi inayoweza kutumika kama malchi (matandazo) na mboji
  • kuongeza unyevunyevu wa udongo kwa kufunikwa kwa matandazo
  • kurejesha bioanuwai kwa kubadilisha mashamba wazi kuwa kilimo msetu
  • kupunguza joto

Muundo wa bustani Msitu: Uzio hai, miti ya mbao, miti ya matunda, miti ya malisho, miti ya kuboresha udongo, na mazao mengi ya chakula kama mahindi, maharage, viazi lishe, mbaazi, muhogo na mbogamboga.

2. Mpangilio wa Miti Kulingana na Eneo

(i) Uzio Hai na Kuzuia Upepo

Grevillea itapandwa kwenye uzio wa bustani ili kusaidia kuzuia upepo na pia kwa mbao.
Nafasi ya kupanda: Panda kwa mita 3 kati ya mche na mche kuzunguka bustani.
Faida: Grevillea hukua haraka na hutoa mbao nzuri, huzuia upepo, ina majani yanayohifadhi unyevu pia ni malisho ya mifugo.

(ii) Miti ya Matunda

Limao, Embe, Parachichi, Fenesi, Papai na Pera
Nafasi ya kupanda: Limao na Pera: mita 4 x 4
Parachichi, Fenesi na Embe: mita 6 x 6
Faida: Matunda ni lishe na soko, kivuli kwa mazao ya chakula pia huchangia katika mfumo wa ikolojia.
Mkadirio ya heka moja: Embe 2, Limao 3, Parachichi 3, Fenesi 1, Pera 3 na Papai 15-50
Upangaji: Panda miti ya matunda ndani ya bustani katika eneo la matunda au pembezoni mwa mazao ya chakula lakini isiwe karibu sana ili yasitengeneze kimvuli kisicho na faida kwenye mazao mengine. Mchanganyiko mzuri ni kuweka miti ya matunda katikati ya mistari ya marejea.

(iii) Miti ya Mbao Ndani ya Bustani

Grevillea, Markhamia, na Cordia zinaweza pia kupandwa ndani ya bustani kwa matumizi ya mbao.
Nafasi ya upandaji: mita 3 x 3 au 5 x 5, kulingana na ukubwa wa bustani na wingi wa miti inayohitajika.
Faida: Kupunguza upepo ndani ya bustani, inatoa majani yanayotengeneza mboji, kutengeneza kivuli chenye faida kwa mazao ya chakulao, malisho ya mifug na baadaye kutoa mbao kwa matumizi ya shambani au biashara.
Mkadirio ya heka moja: Markamia 5, Cordia 5-10, Grevillea 30-99

3. Mpango wa Idadi ya Miche kwa Kila Ukubwa wa Bustani
Mkulima anaweza kurekebisha idadi ya miti kulingana na upatikanaji wa miche na nafasi anayopendelea kutumia kwa mazao mengine.

4. Matunzo ya Miche
Kumwagilia: Mara 3 kwa wiki msimu wa kiangazi.
Kuweka mboji na matandazo: Kila baada ya miezi 3 ili kuboresha rutuba.
Kupogolea: Kupunguza matawi yaliyokufa na kuelekeza matawi juu.
Kulinda dhidi ya wanyama: Funika miche kwa miba, waya au kizuwizi chochote kinachopitisha mwanga.
Udhibiti wa wadudu na magonjwa: Tumia njia za asili kama maji ya pilipili, mwarobaini, tangawizi au majivu.

5. Kuandaa Ramani ya Shamba
Mkulima anatakiwa kuchora ramani ya bustani yake akiainisha mahali pa kupanda miti ya matunda, miti ya mbao, uzio hai na eneo la mazao ya chakula.
Rekodi idadi ya miche iliyopandwa, tarehe ya kupanda na maendeleo ya kila aina ya mti.

6. Mwisho wa Mafunzo na Mazoezi kwa Wakulima
Tathmini: Je, wakulima wanaelewa mpango wa kupanda na kutunza miti yao?
Mazoezi ya vitendo: Kuandaa shamba na kupanda miche ya matunda na mbao kama ilivyo kwenye malengo yao.
Maoni kutoka kwa wakulima: Kusikiliza changamoto zao na kuwashauri zaidi.